MJANE AMTOLEA CHOZI RAIS MAGUFULI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 31 October 2017

MJANE AMTOLEA CHOZI RAIS MAGUFULI

Rais John Magufuli.

Rais John Magufuli amewaaigiza Mkurugenzi Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa, John Mongella na Naibu Waziri wa Ardhi, Angelina mabula kuhakikisha wanashughulikia na kutatua suala la mjane Anna Joyce Francis mkazi wa Isamilo wilayani Ilemela anayedai kudhurumiwa ardhi na mtu aliyemtaja kuwa ni mwanasheria.

Hayo yamejiri leo jijini Mwanza wakati Rais Magufuli akiwahutubia wananchi wa mkoani humo ambako amefanya ziara ya siku mbili kuzindua miundombinu mbalimbali.

“Mhe. Rais mimi ni mjane, nimedhurumiwa ardhi yangu na mwanasheria anaitwa Alex Bandulaki,niliinunua kwa mzawa lakini amekuja anasema aliuziwa na Jiji. Miaka tisa nahangaika amenipeleka mahamani, wanangu wameteseka.

“Barua zangu zimefishwa mahakama ya wilaya anaambiwa ameshinda kesi, hukumu yenyewe ikitoka yake imeandikwa tarehe nyingine na yangu imeandikwa tarehe nyingine,” Mama huyo alilalama huku akimwaga machozi mbele ya Rais.

Baada ya maelezo hayo, Rais alitoa agizo kwa viongozi hao kulishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo ili mama huyo aweze kupata haki yake. Aidha Rais amempa mama huyo kiasi cha fedha kwa ajili ya kujikimu.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewataka Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire na viongozi wenguine wa mkoa huo wamalize malumbano yao ili wawatumikie wananchi.
 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment