MACHUNGUDOA 34 MIKONONI MWA POLISI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 31 October 2017

MACHUNGUDOA 34 MIKONONI MWA POLISI


Kimenuka: Machangudoa 34 Wanaswa Dar es Salaam
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke jijini Dsm Linawashikilia watuhumiwa thelathini na wanne (34) wakiwemo wasichana wadogo zaidi ya ishirini na wanane (28) kwa tuhuma za kufanya biashara ya ngono katika maeneo ya Tandika na Temeke jijini humo ambapo pia polisi wamefunga madanguro yenye vyumba 170 ambavyo vilikuwa vikitumika kwa biashara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Temeke Emmanuel Lukula amesema wasichana hao wenye umri mdogo baadhi wakibainika kuwa wanafunzi ambao wanadaiwa kuletwa na baadhi ya akina mama waendeshaji wa biashara hiyo haramu watafikishwa mahakamani.

Baadhi ya wananchi wamepongeza operesheni hiyo ya kuwaondoa wasichana hao pamoja na kuwakamata baadhi ya wamiliki wa nyumba zinahusika kuwa madanguro ambapo baadhi ya nyumba zimebainika kuwa na vyumba zaidi ya 60 huku chumba kimoja kikiwa na milango miwili mmoja wa mbele na Mmoja wa nyuma ndani kukiwa na kitanda tu.

Mmoja wa wamiliki wa nyumba ambayo inadaiwa ilikuwa ikiendesha biashara hiyo amekiri kujihusisha kwa madai ya kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani jumatatu Octoba 30. like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment