KIGOGO WA CHADEMA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 24 October 2017

KIGOGO WA CHADEMA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI


Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, linamshikilia Mkurugenzi wa Operesheni na mafunzo wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema bwana Kigaila Benson kwa tuhuma za kutoa lugha zinazodaiwa kuwa za kichochezi.


Bw. Kigaila anashiikiliwa kwa tuhuma za kutoa lugha za kichochezi Oktoba 12 katika mkutano wake na waandishi wa habari, na amehojiwa na kunyimwa dhamana ambapo itaamuliwa hapo kesho kupewa dhamana ama kufikishwa mahakamani.
Mwanasheria wa Kigaila Frederick Kihwelo akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo hicho leo Jumatatu amesema hatima ya dhamana ya Mkurugenzi huyo itaamuliwa kesho Jumanne.
Wakili Kihwelo amesema, “Kigaila amehojiwa kwa masaa 3 kuanzia saa 7 mchana hadi saa 10 jioni na amehojiwa kwa makosa aliyoyafanya katika mkutano wake Oktoba 12 na wamekataa kutoa dhamana labda hadi kesho” amesema
Mwanasheria huyo amesema katika mkutano huo alizungumza mambo mengi ikiwemo kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kutekwa kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.


like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment