JPM; OLE WENU MKOPO WA WANAFUNZI UCHELEWESHWE - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 27 October 2017

JPM; OLE WENU MKOPO WA WANAFUNZI UCHELEWESHWERais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa atashangaa sana endapo wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wanastahili kupata mikopo watafungua vyuo na kukosa mikopo hiyo.


Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu Oktoba 27, 2017 na kusema yeye toka tarehe 29 ya mwezi uliopita alikuwa ameidhinisha fedha hizo za mikopo zaidi ya bilioni 145 hivyo anategemea wanafunzi wakifungua vyuo vikuu watapata fedha hizo.


"Toka mwezi uliopita kwenye tarehe 29 nilipitisha bilioni 147 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wanaostahili kupata mikopo, nitashangaa sana kama kutakuwepo na wanafunzi wapo kwenye orodha ya kupata mikopo na mikopo watakuwa hawajapata mpaka wanafungua vyuo, mimi najua nimeshaidhinisha hizo fedha sitapenda kuona wanafunzi wanafungua vyuo na kuanza kuteseka wakati fedha zipo" alisisitiza Rais Magufuli


Vyuo Vikuu nchini Tanzania vinategemewa kufunguliwa mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu kutokana na ratiba iliyotangazwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU)

   like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI