IBRAHIM AJIB KAMA LIONEL MESS - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 16 October 2017

IBRAHIM AJIB KAMA LIONEL MESSIbrahim Ajib ameiga aina ya ushangiliaji wa Lionel Messi katika mechi dhidi ya Kagera Sugar kwenye dimba la Kaitaba siku ya Jumamosi, Octoba 14.

Nyota wa Barcelona, Messi aliwahi kuvua jezi yake na kuinyanyua hewani katika mechi dhidi ya Real Madrid msimu uliopita ambayo Barcelona waliibuka na ushindi wa goli 3 kwa 2 - na Ajib amefanya hivyo wikendi iliyoisha baada ya kufunga goli la ushindi kwa Yanga.

Ibrahim Ajib amefanya kama nyota huyo wa Barcelona kwa kuvua jezi yake na kuionesha hewani kipindi ana shangilia goli lake dhidi ya klabu ya Kagera ambayo Wana Jangwani hao walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa 1 katika mchezo huo wa Ligi Kuu.

Mshambuliaji huyo wa Tanzania, sasa amekuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii baada ya kujaribu kujifananisha na mshindi wa tuzo tano za Ballon d'Or.


Ajibu amefanikiwa kufunga mabao matatu kwenye Ligi Kuu kwa msimu huu.

Yanga wanakamata nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia alama 12 katika michezo 6, pointi sawa na klabu za Simba, Azam, na Mtibwa huku wakitofautiana kwenye magoli ya kufunga na kufungwa.

Aina hii ya ushangiliaji pia imewahi kutumiwa na nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Marcelo katika vipindi tofauti tofauti.like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment