GARI LENYE MWENDO KASI KULIKO YOTE DUNIANI LAANZA MAJARIBIO - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 26 October 2017

GARI LENYE MWENDO KASI KULIKO YOTE DUNIANI LAANZA MAJARIBIO


BLOODHOUND SSC/STEFAN MARJORAMImage captionBloodhound SSC

Gari lililoundiwa nchini Uingereza linaloweza kukimbia kasi ya kilomita 1,610 kwa saa, linafanyiwa majaribio yake ya kwanza huko Cornwall.

Bloodhound SSC linafanya mikimbio ya mwendo wa chini ya hadi kilomita 320 kwa saa katika uwanja wa ndege wa Newquay.
Gari lenye kasi zaidi duniani kujaribiwa Oktoba

Likiendeshwa na Andy Green, gari hilo linalenga kuvunja rekodi ya dunia ya mwendo wa kasi zaidi ardhini.BLOODHOUND SSC/STEFAN MARJORAMImage captionBloodhound SSC

Jaribio hilo litafanywa kwenye barabara maalum iliyojengwa eneo la Nothern Cape nchini Afrika Kusini.

"Tumeunda gari lisilo la kawaida kabisa, lenye uwezo mkubwa na kasi ya juu zaidi katika historia." Andy Green aliambia BBC.

Ni miaka 20 tangu mtu aendeshe gari lenye kasi kubwa duniani katika jangwa la Nevada huko Marekani na kuandisha mwendo wa kilomita 1,227 kwa sasa.BLOODHOUND SSC/STEFAN MARJORAMImage captionBloodhound SSC

Gari hilo jipya limenufaika na teknolojia iliyoboreshwa kwa miongo miwili na litasaidiwa na injini ya ndege ya vita ya Eurofighter-Typhoon ambayo inatumia teknolojia ya roketi.

Bloodhound inataka kufanya jaribio la kuvunja rekodi ya sasa na kuweka kasi kubwa ambayo hakuna mtu anaweza kuifikia au kuitazama.Thrust SSC lilivunja rekodi ya kasi ardhini mwaka 1997like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment