TRUMP AJIPANGA NA KUAPA KUMKABILI KOREA KASKAZINI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Friday, 29 September 2017

TRUMP AJIPANGA NA KUAPA KUMKABILI KOREA KASKAZINIRais wa Marekani Donald Trump atasafiri kuelekea katika mataifa matano ya bara Asia mnamo mwezi Novemba ili kushiriki katika mikutano ya kieneo, Ikulu ya Whitehouse imetangaza.

Atazuru Japan, China, Korea Kusini, Vietnam, Ufilipino na Marekani ya Hawaii kwa ziara ya siku 11.

Ziara hiyo ya marais itaimarisha harakati za kimataifa kukabiliana na tishio la Korea Kaskazini, taarifa hiyo ya Whitehouse imesema.

Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni.

Je maswala muhimu ya rais Trump katika mikutano hiyo yatakuwa nini katika ziara yake ya kwanza bara Asia?
Korea Kaskazini

Taifa hilo ambalo limetengwa kiuchumi lilifanya jaribio lake la sita la kombora la kinyuklia mapema mwezi huu licha ya shutuma za kimataifa, imeahidi kufanya jaribio jingine katika bahari ya pacific.
CHANZO BBC NEWS
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI