MKURUGENZI SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA AHUKUMIWA JELA MIAKA 6 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Wednesday, 13 September 2017

MKURUGENZI SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA AHUKUMIWA JELA MIAKA 6


MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NDEGE ATCL AHUKUMIWA JELA

September 13, 2017 by Global PublishersDavid Mataka.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka na mwenzake Elisaph Mathew, aliyekuwa Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha cha ATCL kwenda jela miaka sita kila mmoja au kulipa faini ya jumla ya Sh. Milioni 70 (Milioni 35 kila mmoja).

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka alipofika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kutolewa hukumu.

Mbali na adhabu hiyo, mahakama pia imewaamuru watuhumiwa hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo ni dola za Marekani 143,442.75 sawa na Sh. Milioni 322.

Aidha mahakama hiyo imemuachia huru William Haji ambaye aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani za ATCL.

Mattaka alipandishwa kizimbani mara ya kwanza mwaka 2008 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi kwa kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni moja zilizotumika kununua magari machakavu.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI