Type something and hit enter

On

 SAIDI KUBENEA MIKONONI MWA POLISI
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea yupo mikononi mwa polisi akisubiri mchakato wa kusafirishwa kupelekwa mjini Dodoma kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Jumanne, Kubenea amesema yupo katika kituo cha polisi cha Oysterbay wilayani Kinondoni na akisubiri utaratibu wa safari ya kwenda Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kama Spika wa Bunge Job Ndugai alivyoagiza.

Kubenea amesema awali kabla ya kushikiliwa alikwenda kujisalimisha polisi katika kituo hicho kisha aliambatana na askari hadi Katika Hospitali ya Aga Khan ambako alitakiwa kwenda kwa ajili ya kufanyiwa kipimo cha MRI.

“Baada ya kipimo kukamilika daktari alishauriwa nipumzike, lakini askari wakaamuru niondoke na kurudi Oysterbay. Hapa ninapozungumza na wewe nipo kituo nikisubiri kusafirishwa kwenda Dodoma,”amesema Kubenea na kuongeza kuwa;

“Hata hivyo, daktari ameshauri nisisafiri kwa njia ya barabara kutokana na matatizo ya mgogo niliyokuwa nayo hivyo nasubiri utaratibu hapa,” amesema mbunge huyo.

Akizungumzia kushirikiliwa kwa Kubenea, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi hilo lilikuwa na hati ya kukamatwa kupelekwa Dodoma kwa mbunge huyo ndiyo maana yupo mikononi mwao.

“Atapelekwa lini, atatoka saa ngapi au atasafirishwa kwa njia gani hilo mimi sijui ila atapelekwa Dodoma chini ulinzi wa polisi. Ukishakuwa na hati ya kukamatwa lazima utakaa mahabusu tu,”amesema Kamanda Mambosasa.

Hata hivyo, Kamanda Mambosasa amesema;“Kwanza sijui kama yupo polisi ndiyo kwanza nakisikia kwako,” alieleza.

Alipotafutwa mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika kujua kama wajumbe wajumbe kamati yake, bado wapo Dodoma baada ya kikao cha Bunge kuhairishwa wiki iliyopita alijibu;

“Shughuli za kamati yangu hazifanyika katika magazeti, sisi tunafanya kimyakimya kisha tunamkabidhi Spika wa Bunge,” alijibu Mkuchika kisha kukata simu.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
Edusportstz
TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
INSTAGRAM
FACEBOOK
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANEL
DOWNLOAD EDUSPORTS ANDROID APPLICATION CLICK HERE
Follow @bakalemwatz
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment