BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 9 September 2017

MANENO YA SAMATTA TUKIO LA LISSUDar es Salaam. Tukio la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jambo hilo limewagusa wachezaji mbalimbali.Wachezaji hao wamekuwa wakutumia akaunti zao za mitandao ya kijamii kumtakia kheri mbunge huyo.


Mbwana Samatta ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuelezea mshtuko wake baada ya tukio hilo.


"Hili ni tukio baya, Tumuombe mheshimiwa Lissu," aliandika nahodha huyo wa Taifa Stars anayeichezea Genk ya Ubelgiji.


Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya aliweka picha ya Lissu kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema anamuomba Mungu ampe nafuu Tundu Lissu.


Mchezaji mwingine aliyeweka picha ya Lissu kwenye ukurasa wake ni kipa wa Simba, Aishi Manula.


Kwa sasa Lissu yuko Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
Edusportstz

No comments:

Post a Comment