LISSU ATARAJIWA KUPELEKWA NAIROBI KWA MATIBABU ZAIDI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Thursday, 7 September 2017

LISSU ATARAJIWA KUPELEKWA NAIROBI KWA MATIBABU ZAIDI


Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Mbunge wa Singida Mashariki ambaye emepigwa risasi na watu wasiojulikana, ametoka chumba cha upasuaji na anatarajiwa kupelekwa Nairobi nchini Kenya.
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara kupitia CHADEMA Mh. Joyce Sokombi ambaye yupo hospitali hapo, amesema kwa sasa Mh. Lissu ametolewa chumba cha upasuaji na anapumzishwa ili kuweza kumsafirisha kwenda Nairobi mara atakapopata fahamu.

"Lissu ameshatoka chumba cha upasuaji na wamempumzisha mpaka atakapoamka, wamsafirishe kwenda Nairobi kwa ajili ya matibabu zaidi, taarifa za matibabu yake zitatolewa na uongozi", alisema Joyce Sokombi.

Tundu Lissu amepigwa risasi leo mchana majira ya saa 7:30 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma, na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ili kunusuru maisha yake.