JEURI LA AZAM KWA SIMBA KUFAMIKA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 8 September 2017

JEURI LA AZAM KWA SIMBA KUFAMIKA

Rekodi ya Azam kwenye Uwanja wa Azam Complex, zinawapa jeuri ya kutamba mbele ya wapinzani wao Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, kesho Jumamosi jioni.


Azam imepoteza michezo minne tu kwenye uwanja wao tangu walipoanza kuutumia mwaka 2011.


Timu ambazo ziliweza kuondoka na pointi tatu kwenye Uwanja wa Azam ni African Lyon kwa ushindi wa bao 1-0 (2011), Mtibwa Sugar kwa ushindi wa 2-1 (2012), JKT Ruvu kwa ushindi wa 1-0 (2014) na Kagera Sugar kwa bao 1-0 mwezi Mei mwaka huu.


Azam kupitia Afisa Habari wake, Jaffer Iddi tayari imetamba kuwa itaituliza Simba na kupanda kileleni mwa msimo wa Ligi Kuu.