BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 4 August 2017

Wezi wa nywele wazua wasiwasi India


Sunita Devi anasema shambulizi hilo limemwaacha na mshutuko

Zaidi ya wanawake 50 katia majimbo yaliyo Kaskazini mwa India ya Haryana na Rajasthan wamesema kuwa wmekatwa nywele zao wakati wakiwa hawana fahamu.

Polis wanajikakamua kutatua visa hivyo ambayo vinawaacha wanawake na mshutuko mkubwa.

"Kulikuwa na mwanga mkali uliosababisha nipoteze fahamu. Saa moja baadaye niligundua kuwa nywele pia ikuwa imekatwa," alisema Sunita Devi, mwamamke mwenye umri wa miak 53 kutoka Haryana.

"Nemeshindwa kulala wala kufanya chochote. Nilisoma kuhusu visa hivi vikifanyika huko Rajasthan, lakini sikufikiria kingetendeka kwangu," aliongeza.Munesh Devi anasema kuna hofu katika jamii

Mbali kidogo mwanamke mwingine Asha Devi naee alipoteza nywele yake katika shambulizi kama hilo siku iliyofuata.

Lakini wakati huo mshambuliaji aliripotiwa kuwa mwanamke.

Baba mkwe wake Asha Devi, Suraj Pal anasema kuwa kufuaia kisa hicho, alimshauri pamoja na wanawake wengine wa familia kuhamia nyumba ya jamaa wao kati jimbo la Uttar Pradesh.Mashambulizi hayo pia yamefanyika mjini Delhi

Bwana Pal anasema alikuwa nyumbani wakati Asha Devi alitoka nje kufanya kazi zake.

"Nilienda nje kujua ni kwa nini hakurudi baada ya zaid ya dakika 30. Tulipata amapoteza fahamu katika chumba cha kuoga. Nyele yake ilikuwa imekatwa na kutupwa sakafuni."alisema.


Ripoti za kunyolewa wanawake kwanza ziliibuka mapema Julai kutoka jimbo la Rajasthan, lakini visa sawa na hivyo kwa sasa vinaripotiwa kutoka Haryan na hata mji mkuu Delhi.Sundar Devi, 60, amekuwa kitandani tangu ashambuliwe Jumamosi

Sunita Devi anaishi katika jamii ya wafanya biashara na wakulima.

Baadhi wa majirani zake wanachukua zamu kukaa naye hadi apate kuondokewa na mshutuko.

Anasema mshambuliaji wake alikuwa ni mwanamume mzee ambaye alikuwa amevaa nguo nyeupe.Wanawake kutokaa sehemu za Delhi wamekuwa wakitumia picha na miungu ili kulinda nywele zoa

No comments:

Post a Comment