BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 5 August 2017

Tahadhari yatolewa kutokana na joto kali Ulaya

Tahadhari yatolewa kutokana na joto kali Ulaya

Jumanne ilikuwa siku yenye joto zaidi mwaka huu Jamhuri ya Czech ambapo joto lilifikia 37C

Baadhi ya maeneo barani Ulaya yanashuhudia viwango vya juu zaidi vya joto katika kipindi cha mwongo mmoja, baadhi ya maeneo vikipokea hadi nyuzi joto 44C (111 F).

Mataifa kadha yametoa tahadhari kwa wakazi wiki hii.

Joto kali nchini Italia limesababisha moto porini na miji kadha imewekwa katika hali ya tahadhari.

Wimbi la joto limesababisha baadhi ya maeneo kukabiliwa na hatari ya ukame mbaya.

43C mjini Roma

Tahadhari ya kiafya imetolewa katika baadhi ya maeneo ambayo viwango vya joto vimepanda kiasi cha kuwa hatari kwa maisha.

Italia inashuhudia viwango vya joto ambavyo ni nyuzi joto 10C juu ya kiwango cha wastani kipindi sawa na cha sasa cha mwaka.

Wananchi wameshauriwa kusalia manyumbani na kunywa maji kwa wingi.

Jumatano, viwango vya joto vilifikia 44C eneo la Sardinia.

Alhamisi, joto lilifikia nyuzi joto 43C karibu na jiji la Roma nako Sicily viwango vya joto vikafikia nyuzi joto 42C huku wingu la hewa yenye joto kali likivuma kutoka Afrika kupitia bahari ya Mediterranean.

Watalii na wenyeji wamekuwa wakipoesha joto kusini mwa Afrika kwa kutumia maji kwenye chemchemi za miji.Watoto walicheza kwenye chemchemi AlbaniaMwanamume atumia maji ya kunywa kupoesha joto midani ya Saint Peter mjini Roma

Hali ya sasa inatarajiwa kuendelea hadi Jumatatu. Hali ya tahadhari imetolewa katika miji 26 Ulaya.Farasi wawili wakimwagiwa maji Vienna, AustriaMtalii Roma akitumia maji kujipoesha kutokana na joto kalihttps://edusportstz.blogspot.com/Mjini Prague, baadhi walitumia fursa ya kuwepo na joto kali kuota jua. Maeneo ya kusini mwa Jamhuri ya Czech yalishuhudia viwango vya joto vya hadi nyuzo joto 38.

No comments:

Post a Comment