Sakata la madiwani wa CHADEMA kuhamia CCM Mbowe anena mazito - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 12 August 2017

Sakata la madiwani wa CHADEMA kuhamia CCM Mbowe anena mazito


Mwenyekiti wa (CHADEMA) na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe amefunguka na kusema ni upambavu mkubwa kutumia zaidi ya milioni mia saba kwa ajili ya kufanya marudio ya uchaguzi wa udiwani wa kata tatu baada ya madiwani wa CHADEMA kudaiwa kununuliwa na CCM.


Mbowe amesema hayo juzi alipokuwa akiongea na wakazi wa Machame Uroki akiwa kwenye ziara yake jimboni Hai na kusema fedha ambazo zinakwenda kwa ajili ya uchaguzi wa marudio zingeweza kufanya mambo mengine ya msingi.


"Gharama ya kurudia uchaguzi wa diwani mmoja ni shilingi milioni mia mbili hamsini, madiwani watatu waliopewa fedha wakaikimbia CHADEMA wakawaacha wananchi huo ni usaliti gharama ya kurudia uchaguzi kwenye kata tatu ni milioni mia saba na hamsini.


"Hizi ni pesa zenu, hizi ni pesa za Watanzania pesa hizi zingetumia kujenga shule ya msingi kwa Kasagile, hizi ni pesa zingetumika kujenga barabara, tunaacha kujenga hospitali tunakwenda kuzitumia fedha hizi kwenye uchaguzi milioni mia saba na hamsini ni upumbavu mkubwa"alisema Mbowe

Hata hivyo Mbowe amesema kuwa licha ya madiwani hao kununuliwa hata uchaguzi ukifanyika kesho anaamini kuwa chama chake kitaibuka na ushindi kwa kata zote tatu

"Niwaambie tu CCM haki ya Mungu hizo Kata tatu haiondoki hata moja labda watu wa Uroki mniambie mko tayari tuwaachie hizo Kata, tutakesha usiku tutakesha mchana haipotei Kata hata moja waite uchaguzi hata kesho, kuna watu wanafika bei tuachane nao tuna mambo ya kupigana katika maisha yetu" alisisitiza Mbowe


Madiwani wa tatu wa jimbo la Hai walijiuzulu nafasi zao na kusema wanamuunga mkono Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano kutokana na utendaji wake madiwani hao ni pamoja na Diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Goodluck Kimaro, Diwani wa Kata ya Weruweru, na Diwani wa Kata ya Mnadani, Everist Peter Kimati ambao wote wamejiunga na CCM.

No comments:

Post a Comment