RIPOTI MPYA YA HALI YA VYOMBO VYA HABARI YAZINDULIWA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Monday, 14 August 2017

RIPOTI MPYA YA HALI YA VYOMBO VYA HABARI YAZINDULIWA


BREAKING: MCT YATANGAZA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA UVAMIZI WA STUDIO ZA CLOUDS TV

August 14, 2017 by Global Publishers
BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limezindua Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari hapa nchini kwa mwaka 2016 (State of the Media Report) ambapo ripoti hiyo hutolewa kila mwaka ili kuushirikisha umma.
Pia Baraza hilo linatoa ripoti kuhusu kuvamiwa kwa Studio za Clouds Media na kubaini jinsi tukio hilo lilivyoathiri uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa uhariri.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Baraza hilo amesema ripoti hiyo haina lengo baya, bali ni kuweka bayana hali ya tasnia ya habari na kwamba hambo hilo si mara ya kwanza kwani baraza hilo limekuwa likitoa ripoti kama hizo kila mwaka.

“Hatujafanya uchunguzi huu kwa kuwa tuna mapenzi na Clouds Media wala kwa sababu tuna mahusiano na Mkuu wa Mkoa, badala yake tumetoa ripoti hii kwa mujibu wa katiba ya MCT,” alisema katibu.