BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 16 August 2017

Rais Lungu: Ni lazima kila mtu apimwe ukimwi
Rais wa Zambia Edga Lungu amesema kuwa kwa sasa ni lazima kila mtu apimwe hali yake ya ugonjwa wa ukimwi nchini humo.

Zambia ni kati ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya ukimwi kusini mwa bara la Afrika kwa asilimia 11.6, huku watu walio na umri wa kati ya miaka 15 na 49, wakiwa na wanaishi na virusi vya ukimwi

Bwana Lungu alisema kuwa kupimwa na kupewa ushauri na matibabu sio kitu cha kujitolea, katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchimi humo.

Alitoa tangazo hilo wakati wa uzinduzi na baraza la ukimwi kwenye mji mkuu Lusaka.

Bwana Lungu alisema kuwa suala hilo limezungumziwa na baraza la mawaziri.

No comments:

Post a Comment