Kwanini Afande Sele aliamua kubaki mwananchi wa kawaida?? - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 15 August 2017

Kwanini Afande Sele aliamua kubaki mwananchi wa kawaida??Afande Sele
Msanii mkongwe wa Hip hop nchini, Afande Sele ambaye hivi karibuni amerudisha kadi yake ya chama cha ACT - Wazalendo, na kuamua kubaki mwananchi wa kawaida huku akiunga mkono kile kinachofanywa na Rais Magufuli, amesema kwa sasa ana imani iko salama

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Afande Sele amesema moja ya sababu ambayo ilimfanya aingie kwenye siasa ni mambo yasiyofaa yaliyokuwa yakifanywa na serikali za awamu zilizopita, huku akiamini anaweza akaleta mabadiliko, lakini kwa sasa haina haja ya yeye kuendelea kufanya hivyo, kwani uongozi uliyopo upo makini.

"Nina amini kabisa mambo mengi ambayo nayatazama kwenye nchi yanavyoendelea sina shaka nayo kabisa kwa sasa. Sababu kubwa iliyonipelekea niingie kwenye siasa ni kutokana na utawala mbovu uliyokuwa katika awamu zilizopita.

Nchi ilikuwa kama Kambale hakuna mtu ambaye anaweza kukemea jambo baya kwa kuwa kila mmoja alijiona mkubwa , nchi ilikuwa inajiendea hovyo hovyo tu. Ndiyo maana nikaamua kuingia kwenye siasa lakini sasa kidogo uliyopo naona unafanya niliyokuwa nayataka", alisema Afande Sele.

No comments:

Post a Comment