BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 27 August 2017

BREAKING: TUNDU LISSU AWATAJA , ATANGAZA MGOMO WA MAWAKILI NA KUTAJA WALIOLIPUA OFISI ZA IMMMARais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Tundu Lissu amewataja watu wanaodaiwa kulipua ofisi za Immma Advocates zilizopo Barabara ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.


Lissu amesema kwamba watu waliovalia sare za polisi, wakiwa na silaha na madumu ya petroli, walivamia ofisi hizo usiku, wakawateka walinzi kabla ya kulipua bomu na kutokomea kusikojulikana.

Aliendelea kueleza kwamba lengo la watu hao lilikuwa ni kuharibu nyaraka muhimu zinazotumiwa na mawakili wanaoongozwa na Fatma Karume na Laurence Masha kwenye kesi mbalimbali zinazoendelea mahakamani, ikiwemo kesi ya Kampuni ya Acacia.

Ofisi hizo zilivamiwa usiku wa saa nane, Agosti 26 ambapo walinzi wawili waliokuwa lindo kwenye ofisi hizo, walitekwa, wakanyweshwa kitu kinachodaiwa kuwa ni sumu na kwenda kutupwa Kawe huku ofisi hizo zikilipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu.

No comments:

Post a Comment