BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 31 August 2017

31 August

NCHI ZENYE MISHAHARA MIKUBWA AFRIKA; TANZANIA IMO

Shirika la Numbeo limetoa orodha ya nchi kumi zenye mishahara mikubwa zaidi barani Afrika. Hili ni shirika kubwa zaidi duniani la ukusanyaji wa taarifa za majiji na nchi. Shirika hili linatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu hali za maisha duniani ikiwemo gharama za maisha, upatikanaji wa nyumba za kupanga, huduma za afya, foleni za barabarani, uhalifu na kiwango cha uchafuzi wa mazingira.

Wednesday, 30 August 2017

30 August

TETESI MICHEZONI LEO TAREHE 30 AUGUST 2017Tottenham wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Argentina Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes kwa pauni milioni 8 na pia bado wanajaribu kumsajili beki wa PSG Serge Aurier, 24, kwa pauni milioni 23. (Guardian)
30 August

OMOG ATABIRI MAKALI JUU YA OKWI MSIMU HUUKocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog.

KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog, amewapa mtihani washambuliaji wake wakiongozwa na Emmanuel Okwi na John Bocco baada ya kusema kuwa, msimu huu anataka kuona timu yake inafunga mabao mengi zaidi ya msimu uliopita ili isitokee wakakosa tena ubingwa kizembe.
30 August

MSUVA:TSHISHIMBI NI KAA LA MOTO


, Simon Msuva.

LICHA ya Yanga kuanza ligi kwa sare, lakini kiungo wa zamani wa timu hiyo, Simon Msuva, ameibuka na kusema kuwa, bado anaipa timu hiyo nafasi ya kutetea ubingwa wake msimu huu.

Tuesday, 29 August 2017

29 August

KIERAN GIBBS MBIONI KUJIUNGA NA WEST BROMKieran Gibbs alicheza mechi 11 Ligi ya Premia msimu uliopita

West Brom wanakaribia kukamilisha ununuzi wa beki wa kushoto wa Arsenal Kieran Gibbs.

Klabu hizo mbili zimeafikiana ada ya £5m kwa mchezaji huyo wa miaka 27 ambaye pia alikuwa akifanya mashauriano na Watford pamoja na klabu ya Galatasaray ya uturuki.

Gibbs bado atahitajika kufanyiwa uchunguzi wa matibabu kabla ya kutia saini mkataba wake.

Kwingineko, Arsenal wamejiunga na Manchester City na Leicester City katika kutaka kumsajili beki wa kati wa West Brom Jonny Evans.

Evans ataruhusiwa kuondoka Hawthorns iwapo tu West brom watafanikiwa kupata mchezaji wa kujaza pengo atakaloacha.

Wanamtaka zaidi mchezaji wa Manchester City Eliaquim Mangala na iwapo Manchester City watamtaka kwa kweli Evans, basi uhamisho huo utakuwa rahisi.


Hata hivyo, Mangala angependa zaidi kujiunga na Inter Milan.

Inter nao zaidi wanataka kumchukua mchezaji wa Arsenal Shkodran Mustafi.

Lakini nao Gunners watakubali tu kumuuza Mustafi iwapo watapata mchezaji wa kujaza pengo atakaloacha, na mchezaji wanayedhani anaweza kufanya hivyo vyema zaidi ni Evans.

West Brom pia wanaweza kufikiria kumnunua nyota wa Liverpool Mamadou Sakho, lakini huenda wakatatizika kufikisha ada yake na mshahara wake.
29 August

MBUNGE WA CHADEMA TUNDUMA ATIWA MIKONONI MWA POLISI

MBUNGE wa Tunduma, Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Mbozi Mjini Vwawa.

Mwakajoka amekamatwa leo Agosti 29 baada ya kufika mahakamani hapo kufuatilia kesi inayomkabili mbunge mwenzake wa Mbozi, Pascal Haonga.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbozi, James Mbasha amesema mbunge huyo amekamatwa lakini hajui kosa linalomkabili. Mbasha amesema alipata taarifa leo asubuhi kwamba mbunge huyo anatafutwa na polisi.

Katika kesi mahakamani hapo, Haonga na wenzake wawili Wilfred Mwalusanya na Mashaka Mwampashi wanakabiliwa na mashtaka mawili, kufanya vurugu na kuwazuia askari kufanya kazi yao kinyume cha sheria.

Mwendesha mashitaka wa polisi, Samwel Saro anadai jana Agosti 28 saa saba mchana, washtakiwa walimzuia askari kutimiza majukumu yake ya kumkamata Mwampashi aliyedaiwa kwamba si mjumbe halali katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo.

Washtakiwa pia wanadaiwa kumfanyia vurugu msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbozi, Lauteri Kanoni.

Washitakiwa walikana mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Asha Waziri ambaye alisema dhamana iko wazi kwa kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka kwa watendaji wa maeneo yao watakaoweka bondi ya Sh2 milioni kila mmoja.

Washtakiwa walitimiza masharti na kuachiwa huru kwa dhamana. Kesi itatajwa Septemba 25 na washtakiwa watasomewa maelezo ya awali.
29 August

BREAKING NEWS:LISSU AONGOZA MGOMO WA MAWAKILI NCHINI

Tundu Lissu akiakiwa na mawakili wengine wakati wakizungumza na wanahabari katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dar.

RAIS wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Tundu Lissu amewaongoza mawakili nchini kugoma kuingia mahakamani kwa muda wa siku mbili Agosti 29 na 30, 2017 wakilaani tukio la kushambuliwa kwa ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA Advocates iliyolipuliwa kwa bomu usiku wa kumakia Jumamosi iliyopita.


“Mengi wamefanyiwa mawakili lakini hili la juzi tumesema hatukubali kukaa kimya wakati mawakili wetu wanashambuliwa. Kwa busara za TLS tuliona tufanye maamuzi ya kusimamisha kazi kwa siku mbili ili kupeleka ujumbe kuwa jambo hilo si jema,” alisema Lissu.

Kuhusu endapo mawakili wote wamegoma Lissu alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa, hadi jioni ambapo ripoti kamili itakuwa imepatikana kwa kuwa kuna mawakili wengine walikuwa na kesi asubuhi, wegine mchana, hivyo haikuwa rahisi kufahamu ni mawakili wangapi wamegoma.
Chanzo: globalpublisher
29 August

SIRI KUFICHUKA BAYANA YA TISHETI NA JINZI LA MANJI
Huku akitia huruma, baadhi ya wananchi jijini hapa wameibua gumzo kuhusiana na nguo anazovaa mfanyabiashara maarufu, Yusufu Manji ambaye ana kesi mbili zinazomkabili. Manji ambaye alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Februari 17, mwaka huu amekuwa akikabiliwa na kesi mbili, moja ikihusu uhujumu uchumi na ya pili ni madai ya matumizi ya dawa za kulevya.

Monday, 28 August 2017

28 August

MSUVA AZIDI KUWEKA REKODI YAKE SAFI LIGI YA MOROCCOWinga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva, jana ameisaidia timu yake, Difaa Hassan El-Jadida kufuzu kwenye Raundi ya Pili ya michuano ya Kombe la Ligi Morocco, maarufu kama Throne Cup baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya CR Khemis Zemamra Uwanja wa Grand Prix mjini Marrakech.
28 August

USIYOYAJUA KUHUSU SOKA LA ULAYA SIKU YA LEO TAR 28 AUGUST 2017Swansea watapanda dau la pauni milioni 13 kutaka kumsajili tena mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony, aliouzwa kwenda City kutoka Swansea mwaka 2015 kwa pauni milioni 28. (Daily Mail)

Inter Milan wanakaribia kumsajili Keita Balde wa Lazio kwa pauni milioni 27. (Daily Mirror)

Birmingham City wanazungumza na kiungo wa kimataifa wa Ghana Afiriye Acquah, 25, kutaka kumsajili kutoka Torino. (Sky Sports

Liverpool wamemuulizia kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21, na wapo tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ya klabu kwa kutoa pauni milioni 55. (Daily Telegraph)

Paris Saint-Germain wamefikia makubaliano ya kumsajili kwa mkopo kwanza, mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, na kuweza kukamilisha usajili wa pauni milioni 166 msimu ujao. (L'Equipe)

Manchester United wamewapa Real Madrid pauni milioni 92 kutaka kumsajili Gareth Bale. (Daily Star)

Barcelona wanamuona Marcus Rashford wa Manchester United kama mrithi wa baadaye wa Luis Suarez. (Don Balon)

Chelsea wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 30 wa kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Daily Telegraph)

Manchester City wapo tayari kuwapa Arsenal pauni milioni 70 pamoja na beki Jason Denayer, ili kumsajili Alexis Sanchez, 28. (Daily Star)

Manchester City wanajiandaa kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang, iwapo watashindwa kumsajili Alexis Sanchez. (Le10Sport)Marcus Rashford na Zlatan Ibrahimovic

Leicester City wamepanda dau la pauni milioni 23 kutaka kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29. (BBC)

Hatma ya meneja wa Crystal Palace iko mashakani baada ya kupoteza mechi tatu za EPL. (Guardian)

Meneja wa West Ham Slaven Bilic anapambana vikali kulinda kazi yake baada ya kupoteza mechi tatu za mwanzo za EPL. (Sun)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema yuko tayari kumruhusu Divock Origi, 22, kuondoka kwa mkopo iwapo klabu yake itaongeza wachezaji wapya kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Liverpool Echo)

Beki wa Arsenal Shkodran Mustafi, 25, anajiandaa kuondoka Emirates na kwenda Inter Milan, mwaka mmoja tu baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 35 kutoka Valencia. (ESPN)Shkodran Mustafi

Stoke City wamefikia makubaliano na Tottenham ya kumsajili beki Kevin Wimmer, 24, kwa pauni milioni 15. (Sky Sports)
28 August

WENGER AWATAKA MASHABIKI KUWA NA AMANIMeneja wa Arsenal Arsene Wenger amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa na imani baada ya kile alichosema kuwa ni uchezaji wa kusikitisha sana baada ya klabu hiyo kucharazwa na Liverpool 4-0 katika mechi ya Ligi ya Premia Jumapili.
28 August

RAIS MAGUFULI AWAIBUKIA TAKUKURU SIKU YA LEO
Ulinzi umeimarishwa katika ofisi za makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) zilizoko Upanga, jijini Dar es Salaam huku ikielezwa kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatembelea ofisi hiyo.

Sunday, 27 August 2017