BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 16 July 2017

TRA Yaongeza Tena Muda wa Kulipa Kodi ya MajengoWakati jana ikiwa ndiyo tarehe ya mwisho wa ulipaji wa kodi za majengo ya mwaka 2016/2017, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imesogeza mbele zoezi hilo hadi Julai 31.

Akizungumza jana Jumamosi, Julai 15, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kuona bado kuna watu wengi wanahitaji kulipia kodi hiyo.

Alisema kwaJiji la Dar es Salaam zimetengwa ofisi maalumu kwa ajili ya kazi hiyo hiyo ili kutoa fursa kwa ofisi nyingine kuendelea kukusanya kodi nyingine.

"Kwa muda mrefu kidogo wahudumu wa TRA wamejikita zaidi kwenye kodi ya majengo, sasa tumeona tutenge maeneo maalumu ili wanaolipa kodi nyingine nao waendelee kuhudumiwa kwa ufanisi," alisema.

Ofisi zitakazoendelea na zoezi hilo kwa Dar es Salaam ni TRA Mbagala, Temeke, Kigamboni, Kimara, Tegeta, Manzese, Ilala, Gerezani, Vingunguti, Samora, Kijitonyama na ofisi ya TRA ndani ya viwanja vya Sabasaba.

Kayombo amesema baada ya Julai 31 watakaolipa kodi hiyo wataambatanisha na faini.

No comments:

Post a Comment