MOURINHO: POGBA LEVO YA MESSI, NEYMAR - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 28 July 2017

MOURINHO: POGBA LEVO YA MESSI, NEYMARKocha wa Manchester United, Jose Mourinho.

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kiungo wake, Paul Pogba yupo katika daraja moja na Lionel Messi na Neymar. Mourinho amesema levo waliopo Messi na Neymar ambao ni mastaa wa Barcelona ni za kipekee na hakuna wengine kama wao lakini Pogba naye yupo katika daraja moja sawa na wao.


Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba.

“Hao ni wachezaji wa kiwango cha kipekee, huwezi kuchukua ubora wao, mmoja wa wachezaji wangu ameonyesha kuwa katika levo sawa na wao,” alisema Mourinho baada ya mchezo wa jana wa timu yake kufungwa bao 1-0 dhidi ya Barcelona.Kabla ya mchezo huo wa kirafiki, Pogba alionekana akiwa karibu na Neymar na walizungumza kwa sekunde kadhaa, baada ya mchezo Pogba akatupia picha mtandaoni ikimuonyesha akibadilishana jezi na Messi huku Neymar akiwa pembeni na wote watatu wakicheka.Baadaye ikaonekana Pogba akimnong’oneza kitu Neymar, mashabiki mitandaoni wakawa wanatania kuwa Pogba ametumwa na kocha wake kumshawishi Mbrazili huyo aelekee Man United badala ya PSG wanaomuwania

No comments:

Post a Comment