BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 23 July 2017

MAAJABU YA DUNIA: MBWA MWENYE PUA MBILI
Pua mbili za mbwa mwenye jina la Toby kama anavyooneakana.
HAYA tunaweza kusema ni maajabu ya dunia, kwa uharisia ni mara chache sana kuona mnyama ambaye viungo vyake vinaonekana kuwa tofauti na wenzke, kama ilivyo kwa binadamu kuwa na kilema kulingana na uumbaji wa Mwenyezi Mungu,Toby ni mbwa mwenye ulemavu wa pua.

Bw. Todd Ray na mbwa huyo.

Mbwa huyo ana pua mbilia, jiulize anapumuaje? Bw. Todd Ray kutoka alikuwa kwenye ufukwe wa Venice huko California, bahati nzuri akiwa anapungwa upepo ufwekuni hapo akamuona mbwa wa maajabu (Toby) akikatisha, kutokana na kuwa na pua mbili Toddy akavutiwa naye na kuamua kumchukua ili amtunze nyumbani kwake.

Todd anasema ‘Kila mtu akimuona Toby anavutiwa– ni mbwa mzuri kuwahi kutokea duniani.’

Mbwa huyo hawezi kunyanyua pua zake juu kwa pamoja wala kuzishusha chini kwa pamoja, lakini ana uwezo wa kunusa vizuri harufu ya mbali kuliko mbwa wa kawaida.

Bw. Todd kwa sasa ameingia kwenye kitabu cha Kumbukumbu za Dunia (Guinness) akiwa na matukio mawili makubwa likiwemo la kufuga wanyama wenye vichwa viwili.

No comments:

Post a Comment