BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 20 July 2017

Katibu Mkuu CHADEMA Dk Vincent Mashinji Apandishwa Kortini na Kisha Kurudishwa RumandKatibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Vincent Mashinji pamoja na viongozi watano wa chama hicho wakiwemo wabunge wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Ruvuma, wakikabiliwa na makosa mawili ikiwemo kufanya mkusanyiko uliotishia usalama wa nchi.


Dk Mashinji alifikishwa mahakamani hapo jana na wanachama wengine watano wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Polisi Songea Mjini.

Walisomewa mashitaka mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kufanya maandamano kinyume cha sheria, ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa nchi.

Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Ruvuma, Simon Kobelo, Wakili Mfawidhi wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Songea, Renatus Mkude alidai Julai 15, mwaka huu mjini Mbamba Bay wilayani Nyasa, washitakiwa walikamatwa na Polisi wakiwa katika maandamano bila kuwa na kibali.

Aidha, Mkude alifafanua kuwa kosa lingine ni kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria, hivyo kuhatarisha usalama wa nchi.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 113 ya mwaka 2017, mbali na Dk Mashinji, washitakiwa wengine ni wabunge Zubeda Sakuro wa Viti Maalumu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini Masasi na mbunge wa Ndanda kupitia chama hicho, Cecil Mwambe.

Wengine ni Katibu wa Ulinzi wa Taifa wa Chadema, Sanuda Madawa, Katibu Mwenezi Kanda ya Kusini Masasi, Charles Makunguru na Katibu wa Chadema Kanda ya Kusini Masasi, Filbert Ngatunga.

Washitakiwa baada ya kusomewa mashitaka yao, walikana kutenda makosa hayo.


Hata hivyo wakati wanasheria wa Chadema wakikamilisha taratibu ya dhamana, Jeshi la Polisi liliwachukua washitakiwa na kuwapandisha kwenye gari na kuwapeleka rumande hadi kesho, ambapo kesi hiyo itatajwa tena.


DK Mashinji na wanachama hao walikamatwa Julai 15, mwaka huu katika mji mdogo wa Mbamba Bay wilayani Nyasa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Nyasa wakiwa katika maandamano na kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria, licha ya serikali kuzuia mikutano yote vyama vya siasa.


Baada ya washitakiwa hao kushikiliwa na polisi wilayani Nyasa kwa saa 48, walipata dhamana kabla ya Jumanne na kupelekwa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa mjini Songea, kabla ya jana kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.


Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Edson Mbogoro ulilalamikia kitendo cha wateja wao, kupelekwa mahabusu kwani hakimu tayari alishatoa ruhusa ya dhamana kwa washitakiwa, jambo ambalo alisema ni kinyume cha taratibu.

No comments:

Post a Comment