BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 30 July 2017

30 July

Maajabu;Daraja refu zaidi la kupitia watu lafunguliwa Uswizi


Daraja lililotundikwa lenye mita 500 linalokisiwa kuwa refu zaidi duniani limefunguliwa katika mji wa Zermatt nchini Uswizi.

Daraja lililotundikwa lenye mita 500 linalokisiwa kuwa refu zaidi duniani limefunguliwa katika mji wa Zermatt nchini Uswizi.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 494 kwa jina Europabrucke limetundikwa mita 85 juu .Daraja hilo lenye urefu wa mita 494 kwa jina Europabrucke limetundikwa mita 85 juu .Daraja hilo linachukua mahala pa daraja jingine ambalo lilikuwa limeharibiwa na mwamba.

Bodi za utalii ya Zermatt inasema kuwa ndio daraja refu zaidi duniani ,ijapokuwa daraja la mita 405 mjini Reutte Austria limetundikwa mita 110 juu kutoka ardhini.

Daraja hilo linachukua mahala pa daraja jingine ambalo lilikuwa limeharibiwa na mwamba.Daraja hilo lipo kati ya Zermatt na Grachen kusini mwa Switzerland.

Daraja hilo jipya ambalo ambalo lina uzito wa tani nane limewekwa kifaa cha ambacho linalizuia kuyumbayumba ,kulingana na bodi ya watalii ya Zermatt.

Daraja hilo lipo kati ya Zermatt na Grachen kusini mwa Switzerland.

Saturday, 29 July 2017

29 July

Bill Gates Kushikilia Ubabe Katika Rekodi Za Matajiri Duniani


Bill Gates ampiku Bezos na kuwa mtu tajiri zaidi dunia

Boss Jeff Bezos alimpiku kwa muda mchache Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani siku ya Alhamisi kufuatia kupanda kwa hisa za mfanyibiashara huyo kabla ya ripoti ya mapato yake ,kabla ya hisa hizo kushuka tena.

Mfanyibiashara huyo ambaye alikuwa nambari nne duniani miongoni mwa watu matajiri zaidi duniani katika kipindi cha mwanzo wa mwaka alimpiku Bill Gates mapema siku ya Alhamisi baada ya hisa zake za kampuni ya Amazon kupanda asilimia 1.8 na kufikia dola 1,071.

Hatahivyo hisa hizo baadaye zilianguka na hivyobasi kufunga zikiwa zimeshuka kwa asilimia 0.7 kwa zikiwa dola 1,046, hatua inayoonyesha kwamba Bezos bado hajamshinda Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani katika orodha ya jarida la Forbes.Bezos sasa ana thamani ya dola bilioni 88.5.

Bei hiyo ya hisa ilijiri saa chache kabla ya Amazon kutangaza mapato ya robo ya mwaka ambapo ilisema kuwa faida imeshuka kwa asilimia 77.

Hii inatokana na hatua yake ya kuimarisha uwekezaji katika video na upanuzi wa kimataifa.

Gates ambaye ana thamani ya dola bilioni 89.7 amekuwa mtu tajiri zaidi duniani tangu mwezi Mei 2013.

Bilionea huyo ametoa dola bilioni 31.1 ya mali yake kwa mashirika ya hisani.

Kwa upande wake Bezos ametoa ufadhili wa dola milioni 100 pekee kulingana na Forbes.

Bezos amekuwa nyuma ya Gates kwa wiki kadhaa, akiwa na thamani ya dola bilioni 89.3 kabla ya kupanda siku ya Alhamisi.Jeff Bezos alimpiku Bill Gates mapema siku ya Alhamisi baada ya hisa zake za kampuni ya Amazon kupanda asilimia 1.8 na kufikia dola 1,071.

Mali yake imeongezeka kwa dola bilioni 24.4 mwaka 2017 huku Amazon ambayo inashilikia asilimia 17 ya hisa zikipanda kwa asilimi 40.

Bezos amempiku bilionea Amancio Ortega ambaye ana thamani ya dola bilioni 82.7 na Warren Buffet mwenye thamani ya bilioni 74.5.

Bilionea huyo wa teknolojia alianzisha kampuni ya Amazon 1994 kama duka la vitabu katika gereji yake mjini Seattle.

Amazon sasa ni mojawapo ya kampuni 50 kubwa duniani ikiwa na duka la mtandaoni na vipindi vya runinga.

Ufanisi wa Amazon Prime, umechangia pakubwa ukuwaji wa kampuni hiyo mwaka huu mbali na umaarufu wa Echo Speaker.

Bezos pia inamiliki gazeti la Washington post na kampuni ya safari za angani Blue Origin.

Pia inamiliki hisa katika kampuni pinzani ya Google, akiwa ndio mtu wa kwanza kuisadia kampuni hiyo ya utafutaji mbali na Airbnb na Uber.
29 July

MSUVA: ASANTENI SANA YANGA



Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva.

NDOTO ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ilitimia juzi Jumatano baada ya kiungo huyo kupaa hadi nchini Morocco kwa ajili ya kumalizana na Difaâ Hassani El Jadidi kabla ya kujiunga nayo rasmi.

Msuva anaikacha Yanga aliyodumu nayo kwa miaka mitano tangu alipoh a mia klabuni hapo akitokea Moro United mwaka 2012, baada y a kukamilika kwa dili hilo ambalo limesimamiwa na meneja wake, Jonas Tiboroha. Ndani ya klabu hiyo ya Difaa El Jadidi, Msuva ataungana na winga, Ramadhan Singano ‘Messi’ ambaye alishatangulia kujiunga na kikosi hicho akitokea Azam FC ambayo alimaliza mkataba.



Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa saba wa Kitanzania kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. Wengine ni Rashid Mandawa aliyepo Botswana, Elias Maguri anayecheza Oman, Thomas Ulimwengu (Sweden), Mbwana Samatta (Ubelgiji), Farid Mussa (Hispania) na Abdi Banda aliyejiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini. M u d a mfupi kabla ya Msuva kukwea pipa kuelekea Morocco juzi Jumatano, Championi Ijumaa, lilipata nafasi ya kuzungumza naye na hapa anafunguka kama ifuatavyo:


Simon Msuva.

NINI UTAKACHOKIKUMBUKA NDANI YA YANGA?

“Daaah! Kuna vitu vingi sana nitavimisi baada ya kuondoka Yanga, siwezi kuvielezea sana lakini kikubwa ni juu ya utani ambao niliuzoea kutoka kwa wachezaji wenzangu, lakini hata kuzurura kwani nilishazoea nikitokea mazoezini naenda maskani ila huko Morocco sidhani kama nitafanya hivyo. “Nikiwa huko nitawakumbuka sana washikaji zangu ambao wamenifanya niwe hapa na wale ambao nimekaa na kushirikiana nao kwa kipindi chote nikiwa Yanga.



UMEJIPANGAJE KUISHI NJE YA TANZANIA?

“Sehemu yoyote ile ukishazoea basi hakuna tatizo lolote lile, najua nitakuwa mgeni kwa siku kadhaa zile za mwanzo lakini baada ya hapo mambo yataenda vizuri. “Itakuwa siyo rahisi kwani huko kila kitu ni kipya ila nitazoea na kuendana na maisha ya huko, kikubwa ni suala la muda tu na kujichanganya na wenzangu.

VIPI KUHUSU LUGHA YAO, INAPANDA? “Sijajua maana nitakuta wanazungumza lugha gani lakini ukija kwenye soka haitakuwa ngumu kuwasiliana na wenzangu kwani mnapokuwa uwanjani mnaongea lugha moja tu ya kimpira. “Shida itakuwa kwenye vitu vingine jinsi ya kuvipata ila uwanjani sitapata sana taabu, lakini kadiri nitakavyokaa ndivyo nitazoea tu sina hofu na hilo.



UNAIONAJE YANGA YA SASA?

“Iko vizuri, hakuna tofauti na timu am
bayo mimi naiacha na ile ya msimu uliopita kwani wachezaji wengi wamebaki na hata kwa wale waliondoka nafasi zao zimezibwa vizuri. “Ukinitoa mimi ninayeondoka naamini hawa waliobaki wataifanya kazi nzuri na kuendeleza mafanikio ambayo tumeyapata wakati ambao nilikuwepo.

UNAJISIKIAJE UNAVYOIACHA YANGA?

“Kiukweli natamani niendelee kuwepo lakini ndiyo hivyo hakuna namna, umeshafika wakati sasa inabidi niondoke kwenda kucheza soka sehemu nyingine tofauti na Yanga. “Najisikia vibaya kuachana na sehemu niliyopata furaha, lakini hakuna namna inanibidi tu niondoke nikatafute maisha sehemu nyingine.

NINI MIPANGO HUKO?

“Nimejipanga kucheza kwa muda mfupi na kwa juhudi kubwa ili nionekane na timu nyingine, sitaki safari yangu iishie Morocco, namaani s h a k w a m b a nitaondoka huko kama nilivyofanya hapa Yanga. “Hiyo ni njia tu ya kwenda kucheza soka Ulaya, kama a m b a v y o n i m e k u w a nikiwaza nifike alipo m s h a m b u l i a j i mwenzangu, Mbwana Samatta ambaye kila mara amekuwa akinipa moyo wa kupambana. Unadhani itakuwa rahisi kutamba Morocco? “Hakuna linaloshindana, naamini kama nikicheza kwa juhudi kubwa na kufuata maelekezo ya kocha atakayonipa basi nina nafasi kubwa ya kuendeleza kile ambacho nimekifanya kwa miaka mitano niliyokaa hapa Yanga,” anasema Msuva.


Friday, 28 July 2017

28 July

Maajabu:Ndege warukao kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kitulo hadi Ulaya



By edusports
Hifadhi ya Taifa Kitulo ndiyo eneo pekee Tanzania lenye ndege aina ya tandawala machaka (Denhams Bustard) wenye uwezo wa kuruka kutoka bara moja hadi jingine
Hifadhi hiyo inayopita katika mikoa ya Mbeya na Njombe ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa mwaka 2005 ikijumuisha sehemu ya eneo la shamba la mifugo, msitu wa Livingstone na bonde la Numbi.
Kitulo ina ukubwa wa kilometa za mraba 442. Awali ilijulikana kama Elton Plateau baada ya Mvumbuzi Fredirick Elton kupita eneo hilo mwaka 1870. Mwaka 1960 Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) lilichukua eneo hilo kwa ajili ya ukulima wa ngano na ufugaji wa kondoo.
Kutokana na umuhimu wa eneo hilo wadau mbalimbali wa mazingira walipendekeza eneo litangazwe kuwa hifadhi ya Taifa ili kulinda umaridadi wa maua, ndege na mimea adimu inayopatikana ndani ya eneo hili.
Dk. Ezekiel Dembe, kaimu mkurugenzi wa Mipango ya Maendeleo na Huduma za utalii katika Hifadhi ya Kitulo anasisitiza kuwa ndege aina ya tandawili machaka hawapatikani sehemu nyingine yoyote hapa Tanzania zaidi ya Kitulo.
Watalii na watafiti wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani hufika katika hifadhi ya Taifa ya Kitulo kwa ajili ya kuwaona ndege hawa ambao wanasafiri umbali mrefu wa kutoka bara moja kwenda bara jingine. 
Dk Dembe anasema ndege hao adimu wanapendwa na watalii wengi duniani na kwamba hifadhi hiyo ndiyo eneo pekee ambalo ndege hao hutaga mayai na kuzaliana kwa wingi kabla ya kusafiri kwenda mabara mengine.
“Utafiti unaonyesha kuna ndege aina ya tandawili machaka ambao waliwekwa alama walipokuwa katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo na baadaye kuonekana wakiwa na alama zao katika hifadhi moja Australia. Utafiti huu ndiyo uliothibitisha kuwa ndege wa aina hiyo wanasafiri kwa kuruka kutoka bara moja kwenda jingine,’’ anasema mhifadhi huyo.
Ndege hao wamekuwa na tabia katika msimu fulani kuruka na kufika katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo kwa ajili ya kutaga mayai na kuangua vifaranga kutokana na mazingira ya hifadhi hiyo kuonekana kuwa ni mahali pekee duniani penye hali ya hewa rafiki kwa ndege hao kuzaliana. Hivyo baada ya kutaga mayai, kuangua vifaranga na ndege kukua, huruka na kwenda mabara mengine duniani.
Utafiti umebaini kuwa katika Hifadhi ya Kitulo ndege aina ya abdims stock, denhams (tandawili machaka) na blue swallow ambao wametoka Afrika Kaskazini, Afrika Kusini, Australia na Ulaya wanaitumia Hifadhi ya Kitulo kama makazi yao katika misimu tofauti.
Watalii wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kitulo wanaweza kuangalia ndege adimu katika Ziwa Zambwe na misitu, kuweka kambi kwa ajili ya malengo mbalimbali, utalii wa kutembea kwa miguu, kupanda farasi, michezo ya gofu na kukwea milima.
Licha ya ndege adimu waliopo, Hifadhi ya Kitulo pia inasifika kwa kuwa na zaidi ya aina 40 za maua mbalimbali ambayo hayapatikani sehemu nyingine yoyote duniani.
Unapoingia katika hifadhi hiyo msimu wa maua kuchanua inakuwa kama vile unga umeanikwa katika miinuko ya hifadhi hiyo hali ambayo inaongeza mvuto kwa watazamaji.
Hifadhi hii imejaliwa kwa kuwa na aina zaidi ya 350 ya mimea ya jamii ya flora.
Mhifadhi Godwel Ole Meing’ataki, Mratibu wa Miradi, mipango ya maendeleo na uboreshaji huduma ya vivutio vya utalii kusini, Spanest anasema katika hifadhi nyingine kuna ujangili, tofauti na Hifadhi ya Kitulo ambako ujangili wake ni wa viazi vya asili (vikanda) ambavyo huchimbwa na kuuzwa nje ya nchi kwa bei kubwa.
Yapo mengi ya kujivunia katika Hifadhi ya Kitulo ukiwamo uwanda wa tambarare, mabonde, vilima na maporomoko ya maji kama Numbi ambako ndani ya msitu kuna miti ya aina ya cidar yenye urefu wa zaidi ya mita 50 na inakadiriwa kuwa ndiyo miti mirefu kuliko yote duniani.
Hifadhi ya Kitulo inafikika kwa gari kutoka Chimala, kilometa 78 Mashariki mwa mji wa Mbeya. Unapanda milima yenye kona 68 ambayo pia ni kivutio hadi katika mji wa Matamba wilayani Makete Mkoa wa Njombe.
Reli ya Tazara hupita karibu na Hifadhi ya Taifa ya kitulo. Pia unaweza kufika ndani ya hifadhi hiyo ukitokea Zambia kupitia Tunduma, ni wastani wa kilometa 170 au Malawi kupitia Wilaya ya Karonga Mkoa wa Mzuzu kwa barabara ni wastani wa kilometa 135.
Kutokea jijini Dar es Salaam kupitia Makambako, Njombe, Makete hadi Kitulo ni wastani wa kilometa 963 na kutoka Dar es Salaam, Chimala, Matamba hadi Kitulo ni wastani wa kilometa 836.
Huduma za hoteli na malazi zinapatikana kwa urahisi katika Jiji la Mbeya ambako kuna hoteli kadhaa zenye hadhi ya kitalii. Pia katika mji wa Matamba ambao upo jirani na hifadhi hii, kuna nyumba za wageni.
Hata hivyo, kutokuwapo kwa juhudi za kutosha katika kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi hiyo kumechangia vivutio vingi vya utalii kutofahamika hata kwa baadhi ya wenyeji.
Uchunguzi umebaini kuwa licha ya Mkoa wa Njombe kuwa na vivutio adimu vya utalii, ikiwamo Hifadhi hiyo ya Kitulo bado wakazi wake hawana mwamko wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo, hali ambayo inachangia kutofahamika kwa vivutio hivyo.
Wananchi walio wengi wanadhani wanaostahili kutembelea vivutio hivyo ni watalii kutoka nje ya nchi pekee. Pia baadhi yao hawajui vivutio vya utalii vilivyopo Njombe wakiamini kuwa fursa ya utalii ipo katika mikoa ya Kaskazini pekee na siyo Kusini.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Allan Kijazi akizungumzia hifadhi za taifa kwa ujumla anasema hadi sasa shirika lake linasimamia hifadhi 16 za taifa ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kukuza pato la taifa.
Kijazi amezitaja changamoto zinazozikabili hifadhi za taifa kuwa ni pamoja na ujangili unaotokana na biashara za kujikimu, upungufu wa maji katika baadhi ya hifadhi wakati wa kiangazi, migogoro ya mipaka katika baadhi ya hifadhi na mwingiliano kati ya wanyamapori na binadamu.

28 July

Shaffih Dauda :urais TFF sasa basi!






Shaffih Dauda ajitoa rasmi kugombea TFF kutokana na nafasi hiyo kumletea mgongano wa kimaslahi na Mwajiri wake.
Shaffih Dauda ametangaza uamuzi huo kupitia kipindi cha 360 cha Clouds TV.
Hata hivyo Shaffih amesema "Nimetumia muda mrefu kujenga Brand yangu hakuna haja kuendelea kung'ang'ania
''Suala la Rushwa ni kunichafua na mimi sitaki''.
28 July

Walovuliwa ubunge waliamsha dudee!!!



Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Lipumba kuwavua uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum kisha Spika Ndugai kuridhia uamuzi huo, jana July 27, 2017
28 July

ZLATAN IBRAHIMOVIC KUREJEA MANCHESTER UNITED

 Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic (Kulia).KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amefunguka kuwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic anaweza kusaini mkataba na timu hiyo. Msimu uliopita mshambuliaji huyo alifanya vizuri na kikosi cha United lakini baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu hakuongezewa mwingine kutokana na kutarajiwa kukaa nje hadi mwakani kutokana na kukumbwa na majeraha ya goti.Kwa sasa United wanatarajiwa kumsimamisha mshambuliaji Romelu Lukaku, kama mshambuliaji wao wa mwisho baada ya kumsajili hivi karibuni akitokea Everton.“Tumetumia fedha nyingi kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji kwa kuwa nafasi hiyo ina vitu viwili, aidha upate mshambuliaji utumie fedha au usimpate. “Lakini pia tumefanya hivyo kwa kuwa tunajua kuwa tutamkosa Zlatan kwa miezi sita ya mwanzoni mwa ligi,” alisema Mourinho. Hii ina maana kuwa Zlatan ambaye msimu uliopita alifanikiwa kuifungia timu hiyo mabao 28, ataisaini mkataba mwingine wa kuitumikia United kwa msimu ujao.

Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic (Kulia).

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amefunguka kuwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic anaweza kusaini mkataba na timu hiyo. Msimu uliopita mshambuliaji huyo alifanya vizuri na kikosi cha United lakini baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu hakuongezewa mwingine kutokana na kutarajiwa kukaa nje hadi mwakani kutokana na kukumbwa na majeraha ya goti.

Kwa sasa United wanatarajiwa kumsimamisha mshambuliaji Romelu Lukaku, kama mshambuliaji wao wa mwisho baada ya kumsajili hivi karibuni akitokea Everton.

“Tumetumia fedha nyingi kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji kwa kuwa nafasi hiyo ina vitu viwili, aidha upate mshambuliaji utumie fedha au usimpate.



“Lakini pia tumefanya hivyo kwa kuwa tunajua kuwa tutamkosa Zlatan kwa miezi sita ya mwanzoni mwa ligi,” alisema Mourinho. Hii ina maana kuwa Zlatan ambaye msimu uliopita alifanikiwa kuifungia timu hiyo mabao 28, ataisaini mkataba mwingine wa kuitumikia United kwa msimu ujao.

Thursday, 27 July 2017

27 July

BREAKING NEWS: NEC YAWATEUA WABUNGE 8 WAPYA WA VITI MAALUM CUF




Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na kifungu cha 86(8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 27 Julai 2017imewateua wafuatao kuwa Wabunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF).
27 July

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 27.07.2017

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 27.07.2017 
Christiano Ronaldo

Wakurugenzi wakuu wa AC Milan Marco Fassone na Massimo Mirabelli wamekutana na wakala Jorge Mendes kumzungumzia Cristiano Ronaldo. Vigogo hao wa Milan wanataka wajulishwe mara tu Ronaldo atakapoweza kupatikana ingawa hakuna majadiliano yoyote kwa sasa. (Sky Sports)

Tottenham wanamnyatia kiungo wa Benfica Ljubomir Fejsa, 28. (Sun)

Meneja wa Everton Ronald Koeman anataka kusajili wachezaji wengine watatu- beki wa kati, mshambuliaji na kiungo mshambuliaji wa Swansea Gylfi Sigurdsson. (Mirror)
Paris Saint_Germain wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 198 wa Neymar, 25, kutoka Barcelona katika siku 15 zijazo. (L'Equipe)
27 July

Lipumba:Maalim Seif ndiye aliyewaponza Wabunge Waliotimuliwa.



Mwenyekiti wa (CUF) anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa Lipumba amefunguka na kusema kuwa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ana kesi ya kujibu na kudai yeye kawaponza wabunge nane waliovuliwa uanachama wa CUF


Profesa Lipumba amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema Katibu Mkuu wa (CUF) Mhe. Maalim Seif na yeye anayake ya kujibu mbele za Kamati ya Maadili na Nidhamu ya CUF.

"Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na kuna wananchama wengine wengi tu ambao pia wana makosa ya kuweza kujibu mbele ya Kamati ya Nidhamu na Maadili katika watu wote hao Katibu Mkuu yumo na yeye ndiye amewaponza hawa wabunge nane wa Viti Maalum ambao wamevuliwa uanachama na ndugu zangu wa Zanzibar na wale wabunge wengine wale msiwe mnasikiliza na kufuata kila anachosema Katibu Mkuu atakuponza kama alivyowaponza wajumbe wa baraza la wawakilishi" alisema Lipumba

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa CUF Taifa Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema mpaka sasa wabunge wote nane ambao wanasemakama wamefukuzwa uanachama wameamua kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga maamuzi feki ambayo yamefanywa na Baraza Kuu feki na kuitaka Mahakama itamke kuwa wao ni wanachama halali wa CUF na wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Lakini pia Katibu Mkuu amesema kuwa Baraza Kuu halali la CUF litakutana kwa dharura siku ya kesho Ijumaa tarehe 28/07/2017 kujadili mambo mbalimbali ambayo yanaendelea katika chama hicho na kutangaza hatua ambazo zitafuata.
Advertisement