Wafungwa 930 watoroka gerezani DRC - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Monday, 12 June 2017

Wafungwa 930 watoroka gerezani DRC


Kumekuwepo na matukio mfululizo ya kuvamiwa kwa magereza na kutoroshwa kwa wafungwa DRC

Gavana wa jimbo la Kivu ya Kaskazini Julien Paluku amesema zaidi ya wafungwa 930 wametoroka baada ya kutokea shambulizi na kuvunja gereza moja huko Congo DRC.

Watu 11 wameuawa katika tukio hilo Kaskazini Mashariki mwa mji wa Beni.

Haijajulikana ni nani haswa aliyefanya shambulizi hilo.

Siku ya Jumamosi wafungwa kadhaa walitoroshwa na mtu mmoja aliyekuwa na silaha.

Mwezi uliopita mamia ya wafungwa walitoroka katika jela moja kubwa mjini Kinshasa baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kuvamia jela hiyo usiku wa manane.
chanzo bbc swahili