Vikosi vya Marekani vyaharibu ngome ya Al-Shabaab Somalia - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Monday, 12 June 2017

Vikosi vya Marekani vyaharibu ngome ya Al-Shabaab Somalia

Linatajwa kuwa miongoni mwa mashambulizi makali dhidi ya Al-Shabaab

Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Farmajo amesema moja ya ngome kubwa za wapiganaji wa Al-Shabaab zimeharibiwa vibaya baada ya shambulizi lililofanywa na vikosi vya Marekani.

Amesema kuwa vikosi maalum vya jeshi la Somalia vinavyopata mafunzo kutoka vile vya Marekani pia vilihusika kuwashambulia Al-Shabaab.

Vikosi vya Marekani vimethibitisha kufanya shambulizi hilo Kusini mwa Somalia.

Haijajulikana kama pametokea uharibifu mwingine wowote.

Siku ya Alhamisi vikosi vya Al-Shabaab viliua watu 59 katika shambulizi kwenye mji wa Puntland Kusini mwa Somalia.