SERIKALI YATANGAZA KUUCHUKUA MSITU WA MWAL NYERERE BUTIAMA. - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 5 June 2017

SERIKALI YATANGAZA KUUCHUKUA MSITU WA MWAL NYERERE BUTIAMA.
Ofisi ya Waziri Mkuu, imesema itaanza kuusimamia na kuutunza msitu wa baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, uliopo Butiama, Mara kama sehemu ya kumuenzi na kuendelea kutunza mazingira.


Hayo yamesemwa jana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika kongamano la mazingira lililofanywa wilayani humo kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya mazingira duniani, yaliyofanyika kitaifa, wilayani Butiama.


“Sisi tutauangalia msitu huu, lakini tunaomba ushirikiano wa wakazi wa Butiama, tukiwaomba wiki hii mfanye kitu hiki, mtusaidie na tushirikiane,” amesema Makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment