BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 5 June 2017

Mbowe afunguka kuhusu sauti inayosambaa mtandaoni…ni yake?
Moja ya story ambayo ina-make headlines kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu sauti (voice note) inayodaiwa kuwa ya Muigazaji Wema Sepetu na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe inayoashiria kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.


New Story leo June 5, 2017 ni kuwa Mbowe kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM ameielezea sauti hiyo akisema taarifa hizo anazichukulia kama majitaka: >>>“Mimi nalichukulia kama taarifa za kawaida za maji taka zinasambazwa. Taarifa ambazo zinatengenezwa hazina ukweli wowote ndio kitu ninachoweza kusema kwa sababu siyo za kweli.

“Timu yangu ya mitandao inajaribu kufuatilia kuhusu kundi ambalo limetengeneza kutuchafua kwani tupo kwenye msiba, kwenye maombolezo na ukweli utajulikana tu muda sio mrefu. Sauti siyo ya kwangu. Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana ni mwanachama wetu na kwamba, kama kuna mahusiano sio kweli, ni taarifa za upotoshaji tu.” – Freeman Mbowe

No comments:

Post a Comment