Jumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi Kenya - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Tuesday, 13 June 2017

Jumba la ghorofa saba laporomoka Nairobi Kenya
Karibu watu 15 hawajulikani waliko baada ya jumba la ghorofa saba kuporomoka usiku wa kuamkia Jumanne, katika kitongoji kimoja cha mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, liliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa makundi ya uokoaji yako eneo la mkasa katika kijiji cha Kware Pipeline mtaa wa Embakasi.

Gazeti la Star nchini Kenya lilisema kuwa watu kadha waliokolewa kabla ya jumba hilo kuporomoka.
Walioshuhudia waliliambia gazeti hilo kuwa jumba hilo lilikuwa limeonyesha dalili baada ya nyufa kuonekana kwenye kuta zake.

Mratibu wa shughuli za uokoaji Pius Masai anasema kuwa zaidi ya watu 100 wanatambulia kuwa salama lakini akaongeza kuwa huenda watu wengi wamekwama.

Idara inayoshughulikia majanga inasema kuwa familia nyingi ziliondoka wakati ziliamriihwa kabla ya jengo hilo halijaporomoka ambapo watu 121 waliondoka salama.

Vyombo vya habari vinasema kuwa baadhi ya watu walirudi tena ndani jengo hilo kuchukua mali yao wakatai liliporomoka.

Polisi wanasema kuwa hawafahamu ni watu wangapi ambao wamekwama ndani ya jengo lililopomoka.

Jumla ya watu 49 walifariki wakati jumba lingine liliporomoka kufuatia mvua kubwa mwezi Aprili mwaka huu.