BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 30 June 2017

30 June

Ujerumani kuichapa Mexico kwa mara ya tatu mfululizo

Siku moja baada ya timu ya taifa ya Ureno kuondolewa katika michuano ya Mabara kwa kufungwa kwa mikwaju ya penati 3-0 dhidi ya timu ya taifa ya Chile katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza, usiku wa June 29 Ujerumani waliingia uwanjani kucheza nusu fainali ya pili dhidi ya Mexico.Mchezo kati ya Ujerumani dhidi ya Mexico ulikuwa ni mchezo ambao unasubiri mshindi ambaye atacheza na Chile katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mabara 2017 inayoendelea nchini Urusi, Ujerumani wamefanikiwa kuingia fainali ya kuifunga Mexico kwa magoli 4-1.Ushindi ambao unakuwa ni watatu mfululizo kwa Ujerumani kupata dhidi ya Mexico wakiwa mara zote wamecheza June 29, toka alipoifunga June 29 1998 katika michuano ya Kombe la Dunia na June 29 2005 katika mchezo wa Kombe la Mabara.Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Leon Goretzka aliyefunga magoli mawili dakika ya 6 na dakika ya 8, Timo Werner dakika ya 89 na Amin Younes dakika ya 90 wakati goli pekee la kufutia machozi kwa Mexico lilifungwa na Marco Fabian dakika ya 89.
30 June

Trump na Putin uso kwa uso wiki ijayo


Trump na Putin walikubaliana kufanya kazi pamoja siku za nyuma

Ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa Rais Donald Trump atakutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wiki ijayo, ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani (G20).

Itakuwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana baina ya viongozi hawa wawili.

Mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani H.R. MacMaster amesema bado hakuna mada maalumu iliyopendekezwa.

Mapema msemaji wa ikulu ya Kremlin alithibitisha uwepo wa mkutano huo.

Thursday, 29 June 2017