Watu 141 mbaroni kwa kuhudhuria sherehe ya wapenzi wa jinsia moja Indonesia - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD EDUSPORTSTS NEWS APP HAPA

Monday, 22 May 2017

Watu 141 mbaroni kwa kuhudhuria sherehe ya wapenzi wa jinsia moja IndonesiaWatu 141 mbaroni kwa kuhudhuria sherehe ya wapenzi wa jinsia moja Indonesia

Polisi nchini Indonesia waliwakamata wanaume 141 ambao walikuwa wanahudhuria sherehe ya wapenzi wa jinsia moja katika mji mkuu wa Jakarta, siku ya Jumapili.

Msemaji wa polisi wa Jakarta Raden Argo Yuwono alisema baadhi ya wale walio kizuizini wanaweza kushtakiwa chini ya sheria kali ya Indonesia ya kupambana na vitendo vichafu.

“Baadhi yao walipatikana wakiwa wamevua nguo na wakishiriki ngono na wengine kujipiga punyeto wakati wa tukio,” aliiambia BBC Indonesia.

Chini ya sheria hizo kali za Indonesia, kuandaa onyesho kama hili ili kuwatumbuiza watu inaweza kufasiriwa kama kosa la kutenda kitendo kichafu eneo la umma.

Sheria kali dhidi ya uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja zilianza kutekelezwa nchini humo mwaka wa 2014.