Wamiliki wa shule wapewa agizo hili na RPC - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 10 May 2017

Wamiliki wa shule wapewa agizo hili na RPC


Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Dhahiri Kidavashari.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari amefunguka na kuwataka wamiliki wa shule mbalimbali jijini humo kuhakikisha magari yao yanayotumika kubeba wanafunzi yanakaguliwa kabla ya kuingia barabarani kutoa huduma hiyo katika shule mbalimbali


Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio, Kidavashari amesema ajali nyingi zinazotokea barabarani ni kutokana na magari hayo kuanza kutoa huduma pasipokuangaliwa badala yake yanakwenda kusababisha vifo na kupoteza rasilimali watu ambayo ndiyo nguvu kazi ya baadaye.

"Wito wangu kwa wamiliki wa shule zote hapa Mbeya magari hayo wahakikishe kwamba yamekaguliwa kabla hayajaingizwa barabarani, na sisi tutafanya zoezi la ukaguzi na kuhakikisha magari hayo ambayo yapo barabarani yanakidhi vigezo vya vbarabarani kwani kinyume na kukidhi vigezo matokeo yake ni vifo na kupoteza rasilimali ambayo ni nguvu kazi ya kesho ambayo ni vijana wetu" alisisitiza RPC, Kidavashari