Tundu Lissu aongea haya kuhusu Siku ya wafanyakazi duniani - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Tuesday, 2 May 2017

Tundu Lissu aongea haya kuhusu Siku ya wafanyakazi duniani


Mmoja wa mawakili wa kujitegemea nchini Bw. Tundu Lissu amewahimiza wafanyakazi nchini kupitia vyama vyao vya wafanyakazi kuhakikisha wanashikamana kudai haki zao za msingi, ili tija wanayotoa iendane na mapato.

Bw. Lissu ameitoa rai hiyo mjini Dodoma, wakati alipokutana na wanachama wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi (TAFETU), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani.

Bw. Lissu ambaye pia ni rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki, amesema umefika wakati sasa kwa shirikisho hilo la (TAFETU) kudai haki za wanachama wao, badala ya kuziomba, kwa sababu ni haki yao.

Mapema akimkaribisha Bw. Lissu kwenye jumuiko hilo, Mwenyekiti wa taifa wa (TAFETU) Bw. Albert Machumu, amesema hakuna haja waajiri kuvichukia vyama vya wafanyakazi nchini, kwa kuwa vyama hivyo vinatekeleza majukumu yake, kwa mujibu wa sheria za nchi.

Shirikisho hilo la (TAFETU) linaundwa na vyama sita, huku kukiwa na vyama vingine 22 visivyo chini ya shirikisho hilo wala lile la (TUCTA).