TAZAMA ALICHOKIANDIKA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA KWENYE "FACEBOOK" - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 10 May 2017

TAZAMA ALICHOKIANDIKA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA KWENYE "FACEBOOK" Kufuatia shughuli za bunge zinazoendelea mjini Dodoma,wabunge wameendelea kuwasilisha michango yao juu ya bajeti zinazowasilishwa bungeni humo.

Leo Jumatano Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ametupia ujumbe kupitia mtandao wa Facebook ukionesha hisia zake juu ya wananchi anaowatumikia. Mheshimiwa Mwigulu amewashukuru wananchi kwa jinsi wanavyomuombea na kumshauri kwa masuala yote yanayohusu Wizara yake ya mambo ya ndani ya Nchi.

"Nawashukuru sana kwa maombi yenu,mawazo,ushauri/maoni yanayohusu hii wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi. Nimeyapokea yote mliyoyaandika na hata yale yaliyowasilishwa na wawakilishi wenu (Wabunge) ndani ya Bunge.....Kifuatacho ni utekelezaji" ameandika waziri Nchemba.No comments:

Post a Comment