RAIS DKT MAGUFULI ATEUA NAIBU KAMISHINA MKUU TRA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 23 May 2017

RAIS DKT MAGUFULI ATEUA NAIBU KAMISHINA MKUU TRA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Uteuzi wa Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru umeanza tarehe 22 Mei, 2017.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru alikuwa Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.

Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Charles Edward Kichere ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa TRA.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment