PICHA 10: Adhabu za Ulaya kwa Madereva wanaopaki magari vibaya - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Saturday, 6 May 2017

PICHA 10: Adhabu za Ulaya kwa Madereva wanaopaki magari vibaya


Kwa Tanzania gari yako ikikutwa imewekwa sehemu isiyotakiwa sanasana wataipiga pini kwa minyororo au kuibeba na wewe utaikuta Manispaa
kwa ajili ya kulipia faini ila kwa wenzetu Ulaya inawezekana tumetofautiana kidogo na ndio maana nimekukusanyia hizi picha 10 za adhabu kwa waliopaki vibaya.
Huyu Jamaa baada ya kupaki vibaya alikuta gari lake limezungushiwa kama hivi ili akome.
Kwenye nchi za Wenzetu miji imepangika kiasi kwamba mabomba ya maji ya kuzimia moto huwa yanawekwa mtaani ili kurahisisha kazi moto ukitokea ambapo huwa ni marufuku kupaki gari karibu na bomba hilo, sasa kilichomkuta huyu jamaa ni Zimamoto kuvunja Vioo vya gari lake ili waweze kupitisha bomba.
Huyu Jamaa aliwekewa vizuizi baada ya kupaki katikati ya barabara.
Huyu Jamaa baada ya kupaki vibaya alikuta gari lake limewekewa uchafu ili akome siku nyingine.
Huyu alikuta amewekewa tuzo ya kuwa dereva mbovu zaidi duniani.
Baada ya kupaki vibaya alikuta madebe ya takataka ili kumuonesha jinsi gani ni dereva mbovu.
Baada ya kupaki vibaya alikuta magari mawili yamemzuia kutoka ili siku nyingine asirudie tena.