Nyumba zateketea kwa moto Sengerema - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 23 May 2017

Nyumba zateketea kwa moto SengeremaSengerema. Nyumba za wavuvi ambazo idadi yake haijajulikana hadi sasa katika kisiwa cha uvuvi cha Nyamango Kata ya Bulyaheke halmashauri ya Buchosa wilayani hapa, zinateketea kwa moto ambapo chanzo chake hakijajulikana.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole umesema moto huo umezuka ulianza saa 8.00 mchana na juhudi za kuuzima zinaendelea kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama.

Kwa mjibu wa mkuu wa wilaya zaidi ya uharibifu wa mali hakuna taarifa ya mtu kupoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo ambalo ni mwendelezo wa matukio kadhaa ya mioto katika visiwa vya uvuvi wilayani humo.

Diwani wa Kata ya Bulyaheke, Bageti Ngele amesema juhudi za wananchi za kudhibiti moto huo hazijazaa matunda kutokana na nyumba hizo kujengwa kwa mbao na mabanzi.

No comments:

Post a Comment