Meli za Magendo ya mafuta,zenye bendera ya Ukraine na Congo zakamatwa Libya - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Tuesday, 2 May 2017

Meli za Magendo ya mafuta,zenye bendera ya Ukraine na Congo zakamatwa Libya

Walinzi wa pwani nchini Libya wamezikamata meli mbili za kigeni na kuwatia mbaroni wafanyakazi wa meli hizo kwa kutuhuma za kufanya magendo ya mafuta kufuatia mapambano ya muda mrefu ya silaha.
Mamla zimesema,Usiku wa alhamisi Walinzi hao walizibaini meli mbili hizo zikiwa zinapeperusha benderza za Ukraine na Congo,takribani kilometa mbili kutoka mji wa Sidi Said karibu na mji wa Zuwara,Magharibi ya pwani ya mji Mkuu Tripoli.

Mkuu wa kikosi hicho,Jenerali Ayoub Qassem,amesema,mapambano baina ya vikosi vyake na watu wenye silaha aina ya Kalashnikovs,waliokuwa kwenye maboti kadhaa yalichukua saa tatu kabla ya kudhibiti hali ya mambo.