-->

Type something and hit enter

On



Ulaji wa nyama hasa nyama nyekundu umekuwa tatizo kubwa sana katika afya zetu kwa hivi karibuni, hata hivyo kuna mjadala wa muda mrefu kuhusu suala la nyama nyekundu, ambapo makundi mawili tofaAuti yamekuwa yakitoleana hoja kuhusu faida na madhara ya kula nyama, hasa ile nyama iliyowekwa katika kundi la ‘nyama nyekundu’ (red meat).

Watalam wa masuala ya afya wanasema kuwa nyama nyekundu huchangia hatari ya mtu kupata ugonjwa wa moyo na saratani ya tumbo, kwani baadhi ya nyama nyekundu huwa na kiwango kikubwa mafuta (saturated fat) ambayo huongeza kolestro mwilini na mtu mwenye kiwango kikubwa cha kolestro huwa hatarini kupatwa na ugonjwa wa moyo.

Kwa upande wa saratani, watafiti wanasema kuwa bado hakujawa na ushahidi wa moja kwa moja kuwa nyama nyekundu inaweza kusababisha saratani ya tumbo. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Afya ya Taifa nchini Marekani, umebaini kuwa watu wanaopenda kula kwa wingi nyama nyekundu, hufa mapema kuliko wale wanaokula kiasi kidogo cha nyama hiyo.

JE, NGURUWE NI NYAMA NYEKUNDU?

Kumezuka swali pia kama nyama ya nguruwe nayo iko kwenye kundi la nyama nyekundu, kwani kimuonekano ni nyeupe.

Jibu ni kwamba nyama ya nguruwe nayo ni nyekundu.
Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo ya Marekani, kiwango cha protini aina ya ‘myoglobin’ kilichomo kwenye misuli ya nyama yoyote ndicho kinachoonesha aina ya nyama. Nyama ya nguruwe inahesabika kuwa ni nyekundu kwa sababu kiwango chake cha ‘myoglobin’ ni kikubwa kuliko kile kilichomo kwenye nyama nyeupe za kuku na samaki.

Kwa ujumla, nyama nyekundu ni muhimu kwa afya ya binadamu, lakini itakuwa muhimu kama itatumiwa kwa kiwango na kiasi kinachotakiwa. Siku zote epuka kula nyama yenye mafuta na badala yake pendelea kula steki isiyokuwa na mafuta ili upate virutubisho vyake muhimu kwa afya yako.

Kula nyama kinyume na mwongozo huu, ni sawa na kuamua kujiweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo na matatizo mengine ya kiafya, ikiwemo ugonjwa wa miguu au kansa ya tumbo. Jiepushe na hayo kwa kuzingatia masharti ya ulaji sahihi.

Click to comment
 
Blog Meets Brand