Kamata kamata Kibiti itaendelea kama kawa: Mwigulu Nchemba - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 24 May 2017

Kamata kamata Kibiti itaendelea kama kawa: Mwigulu Nchemba


Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba amesema kamata kamata itaendelea katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji hadi wahalifu wote watakapokamatwa.

Mwigulu ametoa kauli hiyo leo bungeni, wakati akitoa maelezo ya mauaji yanayoendelea mkoa wa Pwani na kusema kuwa mauaji ya aina hiyo si ya kawaida.

Mwigulu ameyasema hayo baada ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini kuomba Bunge liahirishe shughuli zake ili kujadili hali ya amani katika maeneo hayo.

Selasini amesema kwa sasa watu wanakamatwa hovyo na polisi katika maeneo hayo na kutoa mfano wa kijana Sultan Mpigi aliyekamatwa na polisi mzima lakini maiti yake ilikutwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

No comments:

Post a Comment