BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 31 May 2017

31 May

Magazeti ya Tanzania May 31, 2017

Kaa karibu na edusportstz kupitia mitandaoni ili kupata taarifa punde tu zitufikiapo. ungana nasi kwa kujisajiri kwenye email ili kutumiwa habari zote muhimu.shuka mpaka eneo la jisajiri hapa na ili kutumiwa habari zote zinazobambaTuesday, 30 May 2017

30 May

Atupelee Green katua Singida United


Paul Manjale,Dar Es Salaam.

ALIYEKUWA mfungaji bora wa michuano ya Kombe la FA msimu uliopita,Atupelee Green amejiunga na wageni ligi kuu bara,Singida United akitokea JKT Ruvu ya Pwani.


Taarifa rasmi zinasema Atupelee amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na JKT Ruvu ambayo imeshuka daraja na msimu ujao itacheza ligi daraja la kwanza.


Atupelee anakuwa mchezaji wa pili mzawa kujiunga na Singida United baada ya Kenny Ally Mwambungu aliyejiunga wiki iliyopita akitokea Mbeya City ya mkoani Mbeya.


Kabla ya kutua Singida United,Atupele pia aliwahi kuchezea Coastal Union,Yanga,Kagera Sugar na Ndanda FC ya Mtwara.
30 May

Magazeti ya Tanzania May 30, 2017Kaa karibu na edusportstz kupitia mitandaoni ili kupata taarifa punde tu zitufikiapo. ungana nasi kwa kujisajiri kwenye email ili kutumiwa habari zote muhimu.shuka mpaka eneo la jisajiri hapa na ili kutumiwa habari zote zinazobamba

Monday, 29 May 2017

29 May

Sababu za Banda kuepa Simba
Abdi Banda

Mlinzi kilaka wa klabu ya Simba Abdi Banda amesema anaondoka klabuni hapo kwa kuwa makataba wake umeisha na hakuna mazungumzo yanayoendelea kati yake na uongozi wa wekundu hao, hadi sasa.

Banda, aliwashukuru mashabiki wa Simba na kuwaaga kwenye ukurasa wake wa Instagram, mara baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbao na kutwaa kombe la TFF Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Jumamosi iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dodoma, Banda amesema viongozi wa Simba hawaoneshi kumuhitaji kwani hawajazungumza naye hadi sasa.

"Ni kweli naondoka kwa sababu mkataba wangu umeisha na hakuna kiongozi aliyezungumza na mimi kuhusu mkataba mpya, na ndo maana niliwaaga mashabiki wa Simba kwenye Instagram". Alisema mlinzi huyo wa zamani wa Coastal Union.

Kuhusu wapi anaelekea kwa maisha mapya ya soka, Banda alisema kuwa anataka kuelekea Afrika Kusini kucheza soka huko.
29 May

Lema ataka Manispaa ya Jiji la Arusha ivunjwe


Image result for lema mbunge
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amemuomba Rais John Magufuli kuunda tume ya uchunguzi au avunje halmashauri kutokana madalali kuendelea kukusanya kodi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kutoka kwa wapangaji wa vibanda vinavyomilikiwa na jiji hilo.
29 May

PICHA 9: Kama hukuona alivyoapishwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP Sirro)

Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvua cheo cha Kamishna wa Polisi Simon Sirro na kumvalisha cheo cha Kamishna Generali wa Jeshi la polisi nchini leo Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam


Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Mteule, Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Kamishna Generali wa Jeshi la Polisi Nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaamRais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kufanyia kazi Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro mara baada ya kumuapisha Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaamKamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro akila kiapo cha maadili ya utumishi wa Umma mara baada ya kumuapisha na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaamKamshina wa Polisi nchini Simon Sirro akiandaliwa kwenda kula kiapo mbele ya Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamshina Jenerali wa Polisi nchini leo Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaamRais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, makamu wa Rais Mhe. Samia suluhu Hassan, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Kaimu Jaji Mkuu Profesa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro pamoja na aliyekuwa IGP Ernest Mangu
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, makamu wa Rais Mhe. Samia suluhu Hassan, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro pamoja na aliyekuwa IGP Ernest Mangu pamoja na Makamishna wa PolisiRais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, makamu wa Rais Mhe. Samia suluhu Hassan, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro pamoja na aliyekuwa IGP Ernest Mangu pamoja na Makamishna wa Polisi na maafisa waandamiziRais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro pamoja na aliyekuwa IGP Ernest Mangu. Picha na IKULU.