-->

Type something and hit enter

author photo
By On
Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB
Image result for nomino za kiswahili
Ngeli za Nomino
Katika mada hii utajifunza na kuelewa maana ya ngeli za nomino, utaelewa idadi kamili ya ngeli za nomino katika Kiswahili na maumbo yake. Pia utaweza kutunga sentensi za Kiswahili kwa kutumia ngeli za nomino. Utaelewa pia matumizi ya ngeli za nomino katika lugha.
Malengo:
Baada ya mada hii mwanafunzi atakuwa anafahamu haya yafuatayo:
 • Maana ya ngeli za nomino
 • Idadi ya ngeli za nomino
 • Kutunga sentensi kwa kutumia ngeli za nomino

 Maana ya ngeli za nomino:
Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.  Mfano:
 1. Maji yakimwagika hayazoleki
 2. Mayai yaliyooza yananuka sana
 3. Yai lililooza linanuka sana
 4. Maji liliomwagika halizoleki
Katika mifano hii tunaona kwamba sentensi a, b na c ziko sahihi wakati sentensi d sio sahihi, hii ni kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Kwa maana hiyo sentensi ‘a’ ipo katika ngeli ya YA-YA na senthensi b na c zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentesi d sio sahihi kwa sababu nomino maji haina wingi, kwa hiyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huu ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi.
Jedwali lifuatalo huonesha ngeli za nomino kwa misingi ya upatanisho wa kisarufi.
NGELI UFAFANUZI MIFANO
A-WA

Ngeli hii inahusisha majina ya viumbe hai kama vile wanyama, watu, wadudu, ndege n.k Sungura mjanja ameumia
Sungura wajanja wameumia
Mkuu anawasili
LI-YA

Majina yenye kiambaisha awali li- katika umoja na ya- katika wingi huingia katika ngeli hii Jambia la babu limepotea
Majambia ya babu yamepatikana
KI-VI

Ni ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo k.v, kijito, kilima Chakula kimekwisha
Vyakula vimekwisha
Kijito kimekauka
Vijito vimekauka

U-I

Huwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI(wingi). Pia majina ya baadhi ya viungo vya mwili huingia humu, kewa mfano mkono, mguu, mkia n.k Mlima umeporomoka
Milima imeporomoka
Mkono umevunjika
Mikono imevunjika
Mto huu una mamba wengi
Mito hii ina mamba wengi
U-ZI

Hurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/' k.v ukuta-kuta. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. k.v ufa - nyufa Ukuta umebomoka
Kuta zimebomoka
Wimbo huu unavutia
Nyimbo hizi zinavutia
Ufa umeonekana
Nyufa zimeonekana

I-ZI
Hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (Wingi).

Nyumba imejengwa
Nyumba zimejengwa
Salam imefika
Salam zimefika


U-YA

Ngeli hii inajumuisha nomino ambazo zina kiambishi awali u- katika umoja na ma- katika wingi. Ukuu umekuponza
Makuu yamekuponza
Unyoya unapepea
Manyoya yanapepea

KU

Majina yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina) Kusoma kwako kumekusaidia
Kuchelewa kumemponza
PA/MU/KU-

Huonesha mahali Amekaa pale palipo na wadudu wengi
Amelala mule mulimojaa siafu.
 Amepita kule mbali
Matumizi ya ngeli
 • Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.
 • Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.
 • Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.
 • Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.

Dhana ya O-rejeshi:
O-rejeshi ni kiambishi kinachotumiwa kurejelea kwenye nomono ambayo huwa imetajwa kabla ya kitenzi chenyewe kutajwa. Viambishi hivyo ndivyo vinavyosababisha utegemezi katika sentensi.
Dhima ya muundo wa O-rejeshi
 • Hutumika kama kirejeshi. Kwa mfano; Mtu aliyepigwa jana na wananchi ni mfanyabiashara wa Mwanza.
 •  O-rejeshi hudokeza mahali. Kwa mfano; rudisha ulipokitoa!
 •  O- rejeshi hudokeza wakati. Kwa mfano; Alipokuja alinikuta nimelala.
 • Hutumika kama kiunganishi. Kwa mfano; Alikuja. Nilikuwa nimelala (alipokuja alinikuta nimelala)
 • Hudokeza namna. Mhafano; Kila mtu anashangaa alivyoumia
Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment
 
Blog Meets Brand