SOMA ALICHOPOST HAJI MANARA LEO - EDUSPORTSTZ

Latest

SOMA ALICHOPOST HAJI MANARA LEO


Haji Manara
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Mabingwa wa Ligi Kuu (VPL) Simba SC, Haji Manara amefunguka na kudai anajifahamu yeye binafsi kuwa ndiye msemaji pekee ndani ya wekundu wa Msimbazi na hawezi kusubiri mpaka afe ndio aweze kusifiwa kwa afanyacho.


Manara amesema maneno hayo yenye ukakasi kupitia ukurasa wake wa kijamii huku baadhi ya watu wakimuunga mkono juu ya maneno yake hayo lakini wengine wakionekana kutopendezewa nayo kwa namna moja ama nyingine.

"Sisubiri nife ili mnisifu, najijua 'my self' kuwa mimi ni msemaji wa klabu wa muda wote ndani ya nchi hii ya Tanzania kwa vigezo vyovyote vile hakuna hata wa kukaribia robo. Ukibisha lazima wewe ni mwanga", ameandika Manara.

Kutokana na kauli hiyo ya Manara, baadhi ya wafuasi wake katika mtandao wake wamemuomba kiongozi huyo kumshauri swahiba wake Jerry Muro aweze kurudi katika nafasi yake ya usemaji wa klabu ya Yanga SC ili wapate kujibizana vizuri kama walivyokuwa wanavyofanya hapo awali.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz