SAYANSI ILIYOFICHUKA JINSI MTU ANAVYOANZA MAHUSIANO YA KIMAPENZI - EDUSPORTSTZ

Latest

SAYANSI ILIYOFICHUKA JINSI MTU ANAVYOANZA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

Image result for LOVE
Ishara ya upendo kwa wapendanao
Unapoingia katika mapenzi na mtu ubongo wako unatengeneza mchanganyiko wa kemikali na kuziachia mwilini. Kemikali hizi ni pamoja na Oxytocin, Phenylethylamine na Dopamine. Kemikali hizi huongeza mapingo ya moyo na kusisimua mwili. Na hali hii ndiyo tuyoita mapenzi au mahaba.
Hali hii ni sawa kabisa na ile ambayo watumiaji wa madawa ya kulevya wanaipata.

Kama walevi wa madawa,mtu ambaye ameingia katika mapenzi anaanza kuona vitu tofauti ni uhalisia. Vitu vinaonekana ni vizuri sana na ubaya unajificha kabisa. Unaona vile vitu vizuri tu ambavyo vinakufanya ujisikie vizuri na kupuuza vyote ambavyo vinakufanya ujisikie vibaya.

Ulevi huu unakufanya uone vile vitu ambavyo wewe na mpenzi wako mnafanana na kutupilia mbali vile vyote mnavyotofautiana na vibaya.
Unakufanya pia useme na kufanya vile ambavyo vinampendeza na kumfurahisha mpenzi wako pekee.

Hali hii itaendelea mpaka kilevi kikiisha nguvu na huweza kuchukua muda wa miezi 2 hadi miaka 2. Katika hatua hii, ubongo wako unaaacha kuzalisha kemikali hizi za mapenzi na unajikuta unashangaa ilikuwaje umekuwa na mtu huyo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz