MAGOLI YA BOCCO NA OKWI YALETA MAJANGA UWANJANI, YAIPA SIMBA SARE - EDUSPORTSTZ

Latest

MAGOLI YA BOCCO NA OKWI YALETA MAJANGA UWANJANI, YAIPA SIMBA SARE

Timu ya Simba na All masry zikiwa uwanjani

Wekundu wa msimbazi Simba Jumatano ya March 7 2018 walicheza mchezo wao wa kwanza wa round ya kwanza wa michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry, Simba walikuwa wenyeji wa Al Masry katika mchezo huo uliyochezwa Taifa, Simba wakiwa nyumbani wamelazimishwa sare ya 2-2

Simba walioanza kuziona nyavu za Al Masry mapema tu katika dakika ya 10 kwa nja ya penati, baada ya beki wao kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Haikuchukua muda kwa Al Masry kusawazisha, kwani baada ya kufungwa bao la kwanza walianza mashambulizi makali langoni mwa Simba, na katika dakika ya 11, Ahmed alifunga bao la kusawazisha na kuufanya ubao wa matokeo uwe 1-1.

Mchezo huo ambao Al Masry waliutawala zaidi kipindi cha kwanza, mnamo dakika ya 26 tena walipata bao la pili kwa njia ya penati kupitia Abdalrauf, baada ya Erasto Nyoni kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Simba walikuwa nyuma kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili kilianza mwanzoni kwa Al Masry kuzidi kuonesha uhai, lakini baadaye Simba wakaanza kujibu mashambulizi wakilisakama lango la wapinzani wao, ambapo katika dakika ya 74, Emmanuel Okwi, aliweza kumlaza kwa chenga beki wa Al Masry na kuwa penati ambayo ilizaa bao la pili kwa Simba.

Hali ya uwanja baada ya umeme kukatika na kubadilika kwa hali ya hewa
Baada ya mchezo huo hofu ilitanda uwanjani Mara baada ya kukatika kwa umeme na mvua Kali iliyopelekea kusitisha mchezo huo kwa dakika kadhaa mpaka pali hali ilipotulia.

Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa, Simba SC 2-2 Al Masry SC

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz